prev

Al-A'la

next

1 : 87

سَبِّحِ ٱسۡمَ رَبِّكَ ٱلۡأَعۡلَى

Takasa Jina la Mola wako na kila ushirika na sifa pungufu kwa namna inayonasibiana na utukufu Wake na utakatifu Wake. info
التفاسير: |

2 : 87

ٱلَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ

Mola ambaye ndiye aliyeumba viumbe, Akalitengeneza umbo lao na kulifanya zuri. info
التفاسير: |

3 : 87

وَٱلَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ

Na Aliyekadiria kila kitu na kukipeleka njia inayonasibiana nacho. info
التفاسير: |

4 : 87

وَٱلَّذِيٓ أَخۡرَجَ ٱلۡمَرۡعَىٰ

Na Aliyeotesha nyasi mbichi zenye rangi ya kijani. info
التفاسير: |

5 : 87

فَجَعَلَهُۥ غُثَآءً أَحۡوَىٰ

Akazifanya baadaye kuwa kavu zilizobadilika rangi. info
التفاسير: |

6 : 87

سَنُقۡرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰٓ

Tutakusomea, (ewe Mtume), hii Qur’ani kisomo ambacho hutakisahau. info
التفاسير: |

7 : 87

إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلۡجَهۡرَ وَمَا يَخۡفَىٰ

Isipokuwa iwapo Allah Mtukufu Atataka usahau kwa hekima na maslahi anayoyajua Yeye. Kwani Yeye ni Mjuzi wa yaliyo wazi na yaliyofichika, ya maneno na ya vitendo. info
التفاسير: |

8 : 87

وَنُيَسِّرُكَ لِلۡيُسۡرَىٰ

Na tutakuwepesishia mambo yako yote; miongoni mwayo ni kukusahilishia kubeba majukumu ya utume na kuifanya nyepesi Dini uliyokuja nayo. info
التفاسير: |

9 : 87

فَذَكِّرۡ إِن نَّفَعَتِ ٱلذِّكۡرَىٰ

Basi wakumbushe watu wako, (ewe Mtume), na uwaongoze njia yenye kheri nao, na uwahusu kwa mawaidha yako wale wanaotarajiwa kuwaidhika nayo. Wala usijisumbue kuwashauri wale ambao mawaidha hayawaathiri isipokuwa yanawazidishia ujeuri na kuwafanya wayakimbie. info
التفاسير: |

10 : 87

سَيَذَّكَّرُ مَن يَخۡشَىٰ

Atanufaika kwa mawaidha anayemcha mola wake. info
التفاسير: |
prev

Al-A'la

next
:
0:00 0:00