قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - عبد اللہ محمد اور ناصر خمیس

صفحہ نمبر:close

13 : 67

وَأَسِرُّواْ قَوۡلَكُمۡ أَوِ ٱجۡهَرُواْ بِهِۦٓۖ إِنَّهُۥ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Na yaficheni maneno yenu, (enyi watu), katika jambo lolote miongoni mwa mambo yenu, au yadhihirisheni, kwani yote mawili mbele ya Allah Mtukufu ni sawa. Hakika Yeye, kutakasika ni Kwake, ni Mjuzi wa yaliyomo ndani ya vifua, yatafichika vipi maneno yenu na matendo yenu Kwake? info
التفاسير: |

14 : 67

أَلَا يَعۡلَمُ مَنۡ خَلَقَ وَهُوَ ٱللَّطِيفُ ٱلۡخَبِيرُ

kwani hajui, Mola wa viumbe, viumbe Vyake na mambo yao wakati Yeye Ndiye Aliyewaumba, Akalitengeneza umbo lao na Akalifanya zuri? Na Yeye Ndiye Mpole kwa waja Wake, Ndiye Mwenye kuwatambua wao na matendo yao. info
التفاسير: |

15 : 67

هُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ ذَلُولٗا فَٱمۡشُواْ فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُواْ مِن رِّزۡقِهِۦۖ وَإِلَيۡهِ ٱلنُّشُورُ

Allah Mtukufu Peke Yake Ndiye Aliyewafanyia ardhi iwe nyepesi iliyotayarishwa mpate kutulia juu yake. Basi tembeeni sehemu zake na pande zake na mle riziki ya Allah Mtukufu Anayowatolea humo. Na Kwake Yeye Peke Yake ndio kuna Ufufuzi kutoka makaburini mwenu ili mhesabiwe na mlipwe. Katika hii aya pana ishara ya kuhimiza utafutaji riziki na uchumaji. Pia pana dalili kuwa Allah Mtukufu Ndiye Muabudiwa wa haki Peke Yake Asiye na mshirika, na pana dalili ya uwezo Wake, kukumbusha neema Zake na kuonya kuelemea duniani. info
التفاسير: |

16 : 67

ءَأَمِنتُم مَّن فِي ٱلسَّمَآءِ أَن يَخۡسِفَ بِكُمُ ٱلۡأَرۡضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ

Je mmesalimika, (enyi makafiri wa Makkah), na Allah Mtukufu Aliye mbinguni kuwa Hatawadidimiza ardhini ikawa inatetemeka na nyinyi mpaka mkaangamia? info
التفاسير: |

17 : 67

أَمۡ أَمِنتُم مَّن فِي ٱلسَّمَآءِ أَن يُرۡسِلَ عَلَيۡكُمۡ حَاصِبٗاۖ فَسَتَعۡلَمُونَ كَيۡفَ نَذِيرِ

Au mmesalimika kuwa Allah Mtukufu Aliye juu ya mbingu Hatawatumia upepo wenye kuwapiga mawe madogomadogo? basi mtajua, (enyi makafiri), kua likoje onyo langu kwenu mnapoiona adhabu. Na huko kujua wakati huo hakutawanufaisha. Katika hii aya pana kuthibitisha kuwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Yuko juu kwa namna inayonasibiana na utukufu Wake, kutakasika ni Kwake. info
التفاسير: |

18 : 67

وَلَقَدۡ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ فَكَيۡفَ كَانَ نَكِيرِ

Kwa hakika walikanusha wale waliokuwa kabla ya makafiri wa Makkah kama vile watu wa Nûḥ, ‛Ᾱd na Thamūd walivyowakanusha Mitume wao. Basi kulikuwa namna gani kule kuwakasirikia kwangu na kuwageuzia kwangu neema waliyokuwa nayo kwa kuwateremshia adhabu na kuwaangamiza? info
التفاسير: |

19 : 67

أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ إِلَى ٱلطَّيۡرِ فَوۡقَهُمۡ صَٰٓفَّٰتٖ وَيَقۡبِضۡنَۚ مَا يُمۡسِكُهُنَّ إِلَّا ٱلرَّحۡمَٰنُۚ إِنَّهُۥ بِكُلِّ شَيۡءِۭ بَصِيرٌ

Je kwani walighafilika hawa makafiri wasiwatazame ndege juu yao wakiwa wanazikunjua mbawa zao angani na wakati mwingine wanazikunja na kuzitia mbavuni mwao? Hakuna mwenye kuwahifadhi wasianguke wakiwa katika hali hiyo isipokuwa Mwingi wa rehema. Hakika Yeye Anaona kila kitu, hakuna upungufu wala tofauti. info
التفاسير: |

20 : 67

أَمَّنۡ هَٰذَا ٱلَّذِي هُوَ جُندٞ لَّكُمۡ يَنصُرُكُم مِّن دُونِ ٱلرَّحۡمَٰنِۚ إِنِ ٱلۡكَٰفِرُونَ إِلَّا فِي غُرُورٍ

Bali ni nani huyu ambaye, kulingana na madai yenu, (enyi makafiri), kuwa ni kundi lenu, anayewanusuru asiyekuwa Allah Mtukufu Mwingi wa rehema, iwapo Yeye Atawatakia baya? Makafiri hawakuwa, katika madai yao isipokuwa wako katika kudanganywa na kupotezwa na Shetani. info
التفاسير: |

21 : 67

أَمَّنۡ هَٰذَا ٱلَّذِي يَرۡزُقُكُمۡ إِنۡ أَمۡسَكَ رِزۡقَهُۥۚ بَل لَّجُّواْ فِي عُتُوّٖ وَنُفُورٍ

Bali ni nani huyo mpaji anayedhaniwa atakayewapa nyinyi riziki iwapo Yeye Atazuia riziki Yake na Atawakatalia kuwapa? Bali makafiri wanaendelea kwenye ukiukaji wao na upotevu wao wakiwa katika hali ya ushindani, kujiona na kuikimbia haki, hawaisikii wala hawaifuati. info
التفاسير: |

22 : 67

أَفَمَن يَمۡشِي مُكِبًّا عَلَىٰ وَجۡهِهِۦٓ أَهۡدَىٰٓ أَمَّن يَمۡشِي سَوِيًّا عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Je huyu anayetembea akiwa kichwa chake kimeinama hajui pa kuelekea wala namna ya kutembea ndiye aliyeko kwenye uongofu zaidi au ni yule anayetembea sawasawa? akiwa na kimo kilicholingana, aliye mzima, afuataye njia iliyo ya wazi isiyokuwa na kupinda? Na huu ni mfano Allah Mtukufu Amempigia kafiri na muumini. info
التفاسير: |

23 : 67

قُلۡ هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَكُمۡ وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَٰرَ وَٱلۡأَفۡـِٔدَةَۚ قَلِيلٗا مَّا تَشۡكُرُونَ

Allah Mtukufu Ndiye Aliyewapatisha nyinyi kutoka kwenye hali ya kutokuwako, na akawafanya muwe na masikio ili msikie kwayo, macho ili muonee na nyoyo ili muelewe kwazo. Basi shukrani zenu kwa mola wenu enyi makafiri ni chache sana. info
التفاسير: |

24 : 67

قُلۡ هُوَ ٱلَّذِي ذَرَأَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَإِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ

Waambie, «Allah Mtukufu ndiye Aliyewaumba na Akawaeneza ardhini. Na Kwake Yeye, PekeYake, mtakusanywa baada ya huku kutengana, ili mhesabiwe na mlipwe». info
التفاسير: |

25 : 67

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلۡوَعۡدُ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Na wanasema hao makafiri, «Ni lini itatimia ahadi hii, (ewe Muhammad?) Tupeni habari ya kipindi chake, (enyi Waumini), iwapo nyinyi ni wakweli katika yale mnayoyadai». info
التفاسير: |

26 : 67

قُلۡ إِنَّمَا ٱلۡعِلۡمُ عِندَ ٱللَّهِ وَإِنَّمَآ أَنَا۠ نَذِيرٞ مُّبِينٞ

Waambie hao, (ewe Mtume), «Hakika ujuzi wa kipindi cha kusimama Kiyama uko kwa Allah Mtukufu Peke Yake, Ndiye Anayehusika nacho. Na hakika si lingine ni kwamba mimi ni muonyaji kwenu, ninawaonya na mwisho mbaya wa ukafiri wenu, na ninawaeleza kile Alichoniamrisha Allah Mtukufu nikibainishe upeo wa kubainisha». info
التفاسير: |
next

Al-Mulk

prev
:
0:00 0:00