《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 * - 译解目录

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

含义的翻译 章: 菲里   段:

Surat Al-Fil

أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصۡحَٰبِ ٱلۡفِيلِ
Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo?
Hakika, ewe Muhammad, unajua kwa ujuzi usio ingiliwa na shaka yoyote, alivyo fanya Mola wako Mlezi kuwafanyia wale watu wenye tembo (ndovu), wakataka kuishambulia Nyumba takatifu ya Al-Kaaba.
阿拉伯语经注:
أَلَمۡ يَجۡعَلۡ كَيۡدَهُمۡ فِي تَضۡلِيلٖ
Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika?
Unajua ya kwamba hakika Mwenyezi Mungu amejaalia juhudi yao kutaka kuibomoa Al-Kaaba ivize na ipotelee mbali. Juhudi yao ikapeperuka, na wao wasipate makusudio yao.
阿拉伯语经注:
وَأَرۡسَلَ عَلَيۡهِمۡ طَيۡرًا أَبَابِيلَ
Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi,
Na Mwenyezi Mungu aliwasalitisha na majeshi ya ndege yaliyo watokea makundi kwa makundi yakifuatana, na yakawazunguka kila upande.
阿拉伯语经注:
تَرۡمِيهِم بِحِجَارَةٖ مِّن سِجِّيلٖ
Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni,
Wakiwatupia mawe kutoka Jahannamu.
阿拉伯语经注:
فَجَعَلَهُمۡ كَعَصۡفٖ مَّأۡكُولِۭ
Akawafanya kama majani yaliyo liwa!
Akawafanya kama majani ya mimea yaliyo sibiwa yakatilifu.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 菲里
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 - 译解目录

古兰经斯瓦希里语译解,阿里·穆哈森·伯瓦尼翻译

关闭