Check out the new design

《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 * - 译解目录


含义的翻译 章: 奈拜艾   段:

An-Naba

عَمَّ يَتَسَآءَلُونَ
Wanaulizana kuhusu nini?
阿拉伯语经注:
عَنِ ٱلنَّبَإِ ٱلۡعَظِيمِ
Kuhusu Ile habari kuu.
阿拉伯语经注:
ٱلَّذِي هُمۡ فِيهِ مُخۡتَلِفُونَ
Ambayo kwayo wanahitalifiana.
阿拉伯语经注:
كَلَّا سَيَعۡلَمُونَ
La! Karibu watakuja jua.
阿拉伯语经注:
ثُمَّ كَلَّا سَيَعۡلَمُونَ
Tena la! Karibu watakuja jua.
阿拉伯语经注:
أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ مِهَٰدٗا
Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko?
阿拉伯语经注:
وَٱلۡجِبَالَ أَوۡتَادٗا
Na milima kama vigingi?
阿拉伯语经注:
وَخَلَقۡنَٰكُمۡ أَزۡوَٰجٗا
Na tukakuumbeni kwa jozi?
阿拉伯语经注:
وَجَعَلۡنَا نَوۡمَكُمۡ سُبَاتٗا
Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko?
阿拉伯语经注:
وَجَعَلۡنَا ٱلَّيۡلَ لِبَاسٗا
Na tukaufanya usiku ni nguo?
阿拉伯语经注:
وَجَعَلۡنَا ٱلنَّهَارَ مَعَاشٗا
Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha?
阿拉伯语经注:
وَبَنَيۡنَا فَوۡقَكُمۡ سَبۡعٗا شِدَادٗا
Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu?
阿拉伯语经注:
وَجَعَلۡنَا سِرَاجٗا وَهَّاجٗا
Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto.
阿拉伯语经注:
وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلۡمُعۡصِرَٰتِ مَآءٗ ثَجَّاجٗا
Na tukateremsha maji yanayoanguka kwa kasi kutoka mawinguni.
阿拉伯语经注:
لِّنُخۡرِجَ بِهِۦ حَبّٗا وَنَبَاتٗا
Ili tutoe kwayo nafaka na mimea.
阿拉伯语经注:
وَجَنَّٰتٍ أَلۡفَافًا
Na mabustani yenye miti iliyokamatana.
阿拉伯语经注:
إِنَّ يَوۡمَ ٱلۡفَصۡلِ كَانَ مِيقَٰتٗا
Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake.
阿拉伯语经注:
يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِ فَتَأۡتُونَ أَفۡوَاجٗا
Siku litakapopulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi.
阿拉伯语经注:
وَفُتِحَتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتۡ أَبۡوَٰبٗا
Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango.
阿拉伯语经注:
وَسُيِّرَتِ ٱلۡجِبَالُ فَكَانَتۡ سَرَابًا
Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi.
阿拉伯语经注:
إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتۡ مِرۡصَادٗا
Hakika Jahannamu inangojea!
阿拉伯语经注:
لِّلطَّٰغِينَ مَـَٔابٗا
Kwa walioasi ndio makazi yao.
阿拉伯语经注:
لَّٰبِثِينَ فِيهَآ أَحۡقَابٗا
Wakae humo karne baada ya karne.
阿拉伯语经注:
لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرۡدٗا وَلَا شَرَابًا
Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji.
阿拉伯语经注:
إِلَّا حَمِيمٗا وَغَسَّاقٗا
Ila maji ya moto sana na usaha.
阿拉伯语经注:
جَزَآءٗ وِفَاقًا
Ndio malipo mwafaka.
阿拉伯语经注:
إِنَّهُمۡ كَانُواْ لَا يَرۡجُونَ حِسَابٗا
Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hesabu (juu ya matendo yao).
阿拉伯语经注:
وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا كِذَّابٗا
Na wakakanusha Aya zetu kwa nguvu.
阿拉伯语经注:
وَكُلَّ شَيۡءٍ أَحۡصَيۡنَٰهُ كِتَٰبٗا
Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika.
阿拉伯语经注:
فَذُوقُواْ فَلَن نَّزِيدَكُمۡ إِلَّا عَذَابًا
Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu!
阿拉伯语经注:
إِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ مَفَازًا
Hakika wacha Mungu wanastahiki kufuzu.
阿拉伯语经注:
حَدَآئِقَ وَأَعۡنَٰبٗا
Mabustani na mizabibu.
阿拉伯语经注:
وَكَوَاعِبَ أَتۡرَابٗا
Na wake wazuri waliolingana nao.
阿拉伯语经注:
وَكَأۡسٗا دِهَاقٗا
Na bilauri zilizojaa.
阿拉伯语经注:
لَّا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا كِذَّٰبٗا
Hawatasikia humo upuuzi wala uongo.
阿拉伯语经注:
جَزَآءٗ مِّن رَّبِّكَ عَطَآءً حِسَابٗا
Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha.
阿拉伯语经注:
رَّبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا ٱلرَّحۡمَٰنِۖ لَا يَمۡلِكُونَ مِنۡهُ خِطَابٗا
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, Arrahman (Mwingi wa rehema); hawamiliki usemi mbele yake!
阿拉伯语经注:
يَوۡمَ يَقُومُ ٱلرُّوحُ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ صَفّٗاۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنۡ أَذِنَ لَهُ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَقَالَ صَوَابٗا
Siku atakaposimama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila yule ambaye Mwingi wa rehema atamruhusu, na atasema yaliyo sawa tu.
阿拉伯语经注:
ذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمُ ٱلۡحَقُّۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ مَـَٔابًا
Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anayetaka, na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi.
阿拉伯语经注:
إِنَّآ أَنذَرۡنَٰكُمۡ عَذَابٗا قَرِيبٗا يَوۡمَ يَنظُرُ ٱلۡمَرۡءُ مَا قَدَّمَتۡ يَدَاهُ وَيَقُولُ ٱلۡكَافِرُ يَٰلَيۡتَنِي كُنتُ تُرَٰبَۢا
Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu ataona yale yaliyotangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningelikuwa udongo!
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 奈拜艾
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 - 译解目录

由拉瓦德翻译中心团队与拉布瓦 الدعوة协会和伊斯兰内容服务协会合作翻译。

关闭