পৃষ্ঠা নং:close

9 : 62

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَوٰةِ مِن يَوۡمِ ٱلۡجُمُعَةِ فَٱسۡعَوۡاْ إِلَىٰ ذِكۡرِ ٱللَّهِ وَذَرُواْ ٱلۡبَيۡعَۚ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo! Pindi mwadhini atakapoita kwa ajili ya Swala Siku ya Ijumaa, nendeni upesi msikilize hutuba na mtekeleze Swala, na muache uuzaji na pia ununuaji na kila kinachowashughulisha na hiyo Swala. Hilo mliloamrishwa ni bora kwenu kutokana na yaliyo humo ya kusamehewa dhambi zenu na kupatiwa malipo mema kutoka kwa Allah Mtukufu. Basi iwapo mnayajua manufaa ya nafsi zenu, fanyeni hilo. Kwenye aya hii kuna dalili kua kuhudhuria Swala ya Ijumaa na kusikiliza hutuba ni lazima. info
التفاسير: |

10 : 62

فَإِذَا قُضِيَتِ ٱلصَّلَوٰةُ فَٱنتَشِرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَٱبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِ ٱللَّهِ وَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ كَثِيرٗا لَّعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ

Basi mkisha kuisikia hutuba na mkaitekeleza Swala, tawanyikeni kwenye ardhi na mtafute riziki za Allah Mtukufu, na mtajeni Allah Mtukufu kwa wingi katika hali zenu zote, ili mfaulu kuzipata kheri mbili: za (duniani na za Akhera). info
التفاسير: |

11 : 62

وَإِذَا رَأَوۡاْ تِجَٰرَةً أَوۡ لَهۡوًا ٱنفَضُّوٓاْ إِلَيۡهَا وَتَرَكُوكَ قَآئِمٗاۚ قُلۡ مَا عِندَ ٱللَّهِ خَيۡرٞ مِّنَ ٱللَّهۡوِ وَمِنَ ٱلتِّجَٰرَةِۚ وَٱللَّهُ خَيۡرُ ٱلرَّٰزِقِينَ

Na pindi wanapoona baadhi ya Waislamu biashara au chochote miongoni mwa viliwazo vya duniani na pambo lake, hutawanyika kwenda huko na wakakuacha wewe umesimama juu ya mimbari unatoa hutuba. Waambie, (ewe Nabii), Yaliyoko kwa Allah Mtukufu ya thawabu na neema yana manufaa zaidi kwenu kuliko mambo ya lahwu na biashara. Na Allah Mtukufu, Peke Yake, Ndiye Bora wa wanaoruzuku na kutoa, basi muombeni na mjisaidie kwa kumtii, ili myapate yaliyoko Kwake ya kheri mbili: ya duniani na ya Akhera. info
التفاسير: |
prev

Al-Jumu'ah

next
:
0:00 0:00