വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - അബ്ദുല്ലാഹ് മുഹമ്മദ് & നാസ്വിർ ഖമീസ്.

പേജ് നമ്പർ:close

6 : 60

لَقَدۡ كَانَ لَكُمۡ فِيهِمۡ أُسۡوَةٌ حَسَنَةٞ لِّمَن كَانَ يَرۡجُواْ ٱللَّهَ وَٱلۡيَوۡمَ ٱلۡأٓخِرَۚ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡغَنِيُّ ٱلۡحَمِيدُ

Kwa hakika mlikuwa, (enyi Waumini), na kiigizo chema kwa Ibrãhîm, amani imshukie, na wale waliokuwa naye, kwa anayetumai kupata kheri kutoka kwa Allah Mtukufu duniani na Akhera. Na yoyote anayeyapuuza yale ambayo Allah Mtukufu Anamuitia nayo ya kuwaiga Manabii Wake na akafanya urafiki na maadui Wake, basi Allah Mtukufu Ndiye Mkwasi wa kutowahitajia waja Wake, Ndiye Mwenye kuhimidiwa kwa dhati Yake na sifa Zake, Ndiye Mwenye kushukuriwa kwa namna zote. info
التفاسير: |

7 : 60

۞ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَجۡعَلَ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَ ٱلَّذِينَ عَادَيۡتُم مِّنۡهُم مَّوَدَّةٗۚ وَٱللَّهُ قَدِيرٞۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Huenda Allah Mtukufu Akaweka baina yenu, (enyi Waumini), na wale jamaa zenu washirikina, ambao mlikuwa na uadui nao, mapenzi baada ya machukivu na uwadui kwa kuvifanya vifua vyao viukubali Uislamu. Na Allah Mtukufu ni Muweza wa kila kitu, na Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake, ni Mwingi wa huruma Kwao. info
التفاسير: |

8 : 60

لَّا يَنۡهَىٰكُمُ ٱللَّهُ عَنِ ٱلَّذِينَ لَمۡ يُقَٰتِلُوكُمۡ فِي ٱلدِّينِ وَلَمۡ يُخۡرِجُوكُم مِّن دِيَٰرِكُمۡ أَن تَبَرُّوهُمۡ وَتُقۡسِطُوٓاْ إِلَيۡهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُقۡسِطِينَ

Allah Mtukufu Hawakatazi, (enyi Waumini), kuwakirimu kwa wema makafiri ambao hawakuwapiga vita kwa ajili ya dini wala hawakuwatoa kutoka majumbani mwenu, na kuwafanyia usawa kwa hisani yenu na wema wenu kwao, kwani Allah Mtukufu Anawapenda wale wanaofanya uadilifu katika maneno yao na matendo yao. info
التفاسير: |

9 : 60

إِنَّمَا يَنۡهَىٰكُمُ ٱللَّهُ عَنِ ٱلَّذِينَ قَٰتَلُوكُمۡ فِي ٱلدِّينِ وَأَخۡرَجُوكُم مِّن دِيَٰرِكُمۡ وَظَٰهَرُواْ عَلَىٰٓ إِخۡرَاجِكُمۡ أَن تَوَلَّوۡهُمۡۚ وَمَن يَتَوَلَّهُمۡ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ

Hakika Allah Mtukufu Anawakataza, kuhusu wale waliowapiga vita kwa ajili ya dini na wakawatoa majumbani mwenu na wakawasaidia makafiri kuwatoa nyinyi, kufanya urafiki nao kwa kusaidiana na kupendana. Na yoyote atakayewafanya wao kuwa wasaidizi wake na vipenzi vyake dhidi ya Waumini, basi hao ndio madhalimu wa nafsi zao, wenye kutoka nje ya mipaka ya Allah Mtukufu. info
التفاسير: |

10 : 60

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا جَآءَكُمُ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتُ مُهَٰجِرَٰتٖ فَٱمۡتَحِنُوهُنَّۖ ٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِإِيمَٰنِهِنَّۖ فَإِنۡ عَلِمۡتُمُوهُنَّ مُؤۡمِنَٰتٖ فَلَا تَرۡجِعُوهُنَّ إِلَى ٱلۡكُفَّارِۖ لَا هُنَّ حِلّٞ لَّهُمۡ وَلَا هُمۡ يَحِلُّونَ لَهُنَّۖ وَءَاتُوهُم مَّآ أَنفَقُواْۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ أَن تَنكِحُوهُنَّ إِذَآ ءَاتَيۡتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّۚ وَلَا تُمۡسِكُواْ بِعِصَمِ ٱلۡكَوَافِرِ وَسۡـَٔلُواْ مَآ أَنفَقۡتُمۡ وَلۡيَسۡـَٔلُواْ مَآ أَنفَقُواْۚ ذَٰلِكُمۡ حُكۡمُ ٱللَّهِ يَحۡكُمُ بَيۡنَكُمۡۖ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ

Enyi mliomuamini (Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo)! Wakiwajia wanawake Waumini wakiwa wamehama kutoka nchi ya ukafiri kuja kwenye nchi ya Uislamu, wafanyieni mtihani, ili mjue ukweli wa Imani yao, Allah Mtukufu Ndiye Mjuzi zaidi wa Imani yao. Mkiwajua kuwa ni Waumini kulingana na alama na ushahidi utakaowadhihirikia, basi msiwarudishe kwa waume wao makafiri. Kwani wanawake Waumini si halali waolewe na makafiri, na makafiri si halali wawaoe wanawake Waumini. Nawapeni waume wa wale wanawake waliosilimu mahari waliotoa kuwapa hao wanawake. Na si dhambi kwenu kuwaoa mkiwapa mahari yao. Na msishikilie kuendelea na ndoa za wake wenu waliokufuru. Na takeni kwa washirikina mrudishiwe mahari mliotoa kuwapa wanawake wenu walioritadi na wakaungana na hao washirikina. Na wao watake kurudishiwa mahari waliotoa kwa wanawake wao waliosilimu na wakaungana na nyinyi. Hukumu hii iliyotajwa katika aya hii ni hukumu ya Allah Mtukufu Anahukumu baina yenu, basi msiende kinyume nayo. Na Allah Mtukufu ni Mjuzi, hakuna kitu chochote kinachofichika Kwake, ni Mwingi wa hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake. info
التفاسير: |

11 : 60

وَإِن فَاتَكُمۡ شَيۡءٞ مِّنۡ أَزۡوَٰجِكُمۡ إِلَى ٱلۡكُفَّارِ فَعَاقَبۡتُمۡ فَـَٔاتُواْ ٱلَّذِينَ ذَهَبَتۡ أَزۡوَٰجُهُم مِّثۡلَ مَآ أَنفَقُواْۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ ٱلَّذِيٓ أَنتُم بِهِۦ مُؤۡمِنُونَ

Na pindi baadhi ya wake zenu wanaporitadi na kujiunga na makafiri, na makafiri wasiwape mahari mliyotoa kuwapatia hao wanawake, kisha mkapambana na hao makafiri na kupata ushindi juu yao, basi wapeni wale Waislamu, ambao wake zao waliondoka, kitu katika ngawira au kinginecho kama kile cha mahari walichowapa kabla ya hapo. Na muogopeni Allah Mtukufu mnayemuamini. info
التفاسير: |
prev

Al-Mumtahanah

next
:
0:00 0:00