قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - عبد اللہ صامت اور ناصر خمیس * - ترجمے کی لسٹ


معانی کا ترجمہ سورت: سورۂ نازعات   آیت:

Surat An-Nazi'at

وَٱلنَّٰزِعَٰتِ غَرۡقٗا
Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Malaika ambao huzing’oa roho za makafiri mng’oo mkali.
عربی تفاسیر:
وَٱلنَّٰشِطَٰتِ نَشۡطٗا
Na kwa Malaika ambao huzitukua roho za Waumini kwa uchangamfu na upole.
عربی تفاسیر:
وَٱلسَّٰبِحَٰتِ سَبۡحٗا
Na kwa Malaika wanaoogelea katika kushuka kwao kutoka mbinguni na kupaa kwao kwenda mbinguni.
عربی تفاسیر:
فَٱلسَّٰبِقَٰتِ سَبۡقٗا
Na kwa Mlaika ambao wanakimbilia kutekeleza amri za Mwenyezi Mungu.
عربی تفاسیر:
فَٱلۡمُدَبِّرَٰتِ أَمۡرٗا
Na kwa Malaika wanaopitisha amri za Mola wao katika mambo ya ulimwengu waliowakilishwa kuyafanya na kuyasimamia, - Wala haifai kwa kiumbe kukiapia chochote kile, bali yapasa kiapo chake kiwe ni kwa jina la Mola wake Muumba au sifa Zake. Na lau ataapa kwa asiye Muumba wake, basi huyo amekuwa mshirikina - Watafufuliwa viumbe bila shaka na watahesabiwa.
عربی تفاسیر:
يَوۡمَ تَرۡجُفُ ٱلرَّاجِفَةُ
Siku ambayo ardhi itatetemeka kwa mvuvuo wa kwanza:
عربی تفاسیر:
تَتۡبَعُهَا ٱلرَّادِفَةُ
mvuvio wa kufisha, ukifuatiwa na mvuvio mwingine wa kuhuisha.
عربی تفاسیر:
قُلُوبٞ يَوۡمَئِذٖ وَاجِفَةٌ
Nyoyo za makafiri, Siku hiyo, zitakuwa na papatiko kwa kicho kikubwa.
عربی تفاسیر:
أَبۡصَٰرُهَا خَٰشِعَةٞ
Macho ya makafiri hao yatakuwa madhalilifu kwa kitisho watakachokiona.
عربی تفاسیر:
يَقُولُونَ أَءِنَّا لَمَرۡدُودُونَ فِي ٱلۡحَافِرَةِ
Wanasema hawa wakanushao kufufuliwa:
عربی تفاسیر:
أَءِذَا كُنَّا عِظَٰمٗا نَّخِرَةٗ
«Je, tutarudishwa baada ya kufa kwetu kwenye yale tuliyokuwa nayo katika ardhi? Je, tutarudishwa na hali tushakuwa mifupa iliochakaa?»
عربی تفاسیر:
قَالُواْ تِلۡكَ إِذٗا كَرَّةٌ خَاسِرَةٞ
Wakasema: «Kurejea kwetu huko kutakuwa kutupu kusikokuwa kweli.’
عربی تفاسیر:
فَإِنَّمَا هِيَ زَجۡرَةٞ وَٰحِدَةٞ
Hakika tukio hilo litakuwa kwa mvivio mmoja tu.
عربی تفاسیر:
فَإِذَا هُم بِٱلسَّاهِرَةِ
Wakitahamaki wao wako hai juu ya ardhi baada ya kuwa walikuwa ndani yake.
عربی تفاسیر:
هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ
Je imekujilia, ewe Mtume, habari ya Mūsā?
عربی تفاسیر:
إِذۡ نَادَىٰهُ رَبُّهُۥ بِٱلۡوَادِ ٱلۡمُقَدَّسِ طُوًى
Pindi Mola wake Alipomwita katika bonde lililotakaswa na kubarikiwa, la Ṭuwā. Akamwambia:
عربی تفاسیر:
ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ
«Enda kwa Firauni. Hakika yeye amekiuka mno katika kuasi.
عربی تفاسیر:
فَقُلۡ هَل لَّكَ إِلَىٰٓ أَن تَزَكَّىٰ
Ukamwambie, ‘Je, unapendelea kuitakasa nafsi yako na upungufu na kuipamba na imani?
عربی تفاسیر:
وَأَهۡدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخۡشَىٰ
Na nikuelekeze njia ya kumtii Mola wako, upate kumcha na kumuogopa?’»
عربی تفاسیر:
فَأَرَىٰهُ ٱلۡأٓيَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰ
Mūsā alimuonyesha Firauni alama kubwa: fimbo na mkono.
عربی تفاسیر:
فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ
Hapo Firauni alimkanusha Nabii wa Mwenyezi Mungu , naye ni Mtume Mūsā, amani imshukie, na alimuasi Mola wake Aliyetukuka.
عربی تفاسیر:
ثُمَّ أَدۡبَرَ يَسۡعَىٰ
Kisha alikengeuka hali ya kuipa mgongo Imani na kufanya bidii katika kumpinga Mūsā.
عربی تفاسیر:
فَحَشَرَ فَنَادَىٰ
Hapo aliwakusanya raia wa utawala wake na akawaita kwa
عربی تفاسیر:
فَقَالَ أَنَا۠ رَبُّكُمُ ٱلۡأَعۡلَىٰ
kuwaambia,»Mimi ndiye mola wenu ambaye hakuna mola mwengine aliye juu yake.»
عربی تفاسیر:
فَأَخَذَهُ ٱللَّهُ نَكَالَ ٱلۡأٓخِرَةِ وَٱلۡأُولَىٰٓ
Hapo Mwenyezi Mungu Alimtesa kwa adhabu ya duniani na ya Akhera.
عربی تفاسیر:
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّمَن يَخۡشَىٰٓ
Na Akaifanya adhabu hiyo iwe ni mazingatio na ni onyo kwa watu mfano wake kati ya wale waasi. Hakika Firauni na kile kilichompata cha adhabu ni mawaidha kwa mwenye kuwaidhika na kutishika.
عربی تفاسیر:
ءَأَنتُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَمِ ٱلسَّمَآءُۚ بَنَىٰهَا
Je, kufufuliwa kwenu, enyi watu, baada ya kufa ni kugumu zaidi, katika vipimo vyenu, au ni kuumbwa kwa mbingu?
عربی تفاسیر:
رَفَعَ سَمۡكَهَا فَسَوَّىٰهَا
Amezipanga juu yenu kama jengo. Na Ameinua sakafu yake angani, haina tofauti wala nyufa.
عربی تفاسیر:
وَأَغۡطَشَ لَيۡلَهَا وَأَخۡرَجَ ضُحَىٰهَا
Na Ameutia giza usiku wake kwa kutwa kwa jua lake. Na Ameweka wazi mchana wake kwa kuchomoza kwake.
عربی تفاسیر:
وَٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ ذَٰلِكَ دَحَىٰهَآ
Na ardhi baada ya kuumba mbingu Ameitandaza. Na Ameweka humo manufaa yake.
عربی تفاسیر:
أَخۡرَجَ مِنۡهَا مَآءَهَا وَمَرۡعَىٰهَا
Na Ametumbua humo chemchemu za maji. Na Ameotesha humo mimea inayolishwa.
عربی تفاسیر:
وَٱلۡجِبَالَ أَرۡسَىٰهَا
Na Ameyakita humo majabali yakiwa ni vigingi vyake. Ameumba, Aliyetakasika na kila upungufu,
عربی تفاسیر:
مَتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ
neema zote hizi zikiwa ni manufaa kwenu na kwa wanyama wenu. (Hakika kurudisha kuumbwa kwenu, Siku ya Kiyama, ni sahali kwa Mwenyezi Mungu kushinda kuumba viumbe hivyo vyingine. Na vyote hivyo, kwa Mwenyezi Mungu, ni rahisi na ni vipesi).
عربی تفاسیر:
فَإِذَا جَآءَتِ ٱلطَّآمَّةُ ٱلۡكُبۡرَىٰ
Pindi kitakapokuja Kiyama Kikubwa na balaa nzito, nao ni Mvuvio wa pili. Kipindi hicho zitaoneshwa kwa binadamu vitendo vyake vyote, za kheri na za shari.
عربی تفاسیر:
يَوۡمَ يَتَذَكَّرُ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا سَعَىٰ
Hapo atazikumbuka na kuzitambua.
عربی تفاسیر:
وَبُرِّزَتِ ٱلۡجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ
Na utaoneshwa Moto wa Jahanamu kwa kila aonaye, uwe waonekana waziwazi.
عربی تفاسیر:
فَأَمَّا مَن طَغَىٰ
Ama yule atakayekiuka amri ya Mwenyezi Mungu
عربی تفاسیر:
وَءَاثَرَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا
na akapendelea maisha ya ulimwenguni kuliko ya Akhera,
عربی تفاسیر:
فَإِنَّ ٱلۡجَحِيمَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ
basi kwa kweli marejeo yake ni Motoni.
عربی تفاسیر:
وَأَمَّا مَنۡ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ وَنَهَى ٱلنَّفۡسَ عَنِ ٱلۡهَوَىٰ
Na ama yule atakayeogopa kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu kuhesabiwa na akaikanya nafsi yake na matamanio mapotofu,
عربی تفاسیر:
فَإِنَّ ٱلۡجَنَّةَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ
basi Peponi ndiko makazi yake.
عربی تفاسیر:
يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرۡسَىٰهَا
Wanakuuliza washirikina, ewe Mtume, kwa madharau, kuhusu wakati wa kuanzia Kiyama unachowaonya.
عربی تفاسیر:
فِيمَ أَنتَ مِن ذِكۡرَىٰهَآ
Wewe huna kamwe ujuzi nacho.
عربی تفاسیر:
إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَىٰهَآ
Bali mambo ya ujuzi huo yarejeshwe kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye Sifa Tukufu.
عربی تفاسیر:
إِنَّمَآ أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخۡشَىٰهَا
Wewe linalokuhusu katika habari zake ni kumuonya nacho yule anayekiogopa.
عربی تفاسیر:
كَأَنَّهُمۡ يَوۡمَ يَرَوۡنَهَا لَمۡ يَلۡبَثُوٓاْ إِلَّا عَشِيَّةً أَوۡ ضُحَىٰهَا
Kama kwamba wao siku watakapouona Kiyama kimesimama, watakuwa hawakukaa katika maisha yao ya duniani, kwa vituko vya hiko Kiyama, isipokuwa ni kama kwamba wamkaa kati ya adhuhuri mpaka kutwa juwa, au ni kama kati ya kuchomoza jua mpaka nusu ya mchana.
عربی تفاسیر:
 
معانی کا ترجمہ سورت: سورۂ نازعات
سورتوں کی لسٹ صفحہ نمبر
 
قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - عبد اللہ صامت اور ناصر خمیس - ترجمے کی لسٹ

قرآن کریم کے معانی کا سواحلی ترجمہ ڈاکٹر عبد اللہ محمد ابو بکر اور شیخ ناصر خمیس نے کیا ہے۔

بند کریں