prev

An-Nazi'at

next

1 : 79

وَٱلنَّٰزِعَٰتِ غَرۡقٗا

Anaapa Allah Mtukufu kwa Malaika ambao huzing’oa roho za makafiri mng’oo mkali. info
التفاسير: |

2 : 79

وَٱلنَّٰشِطَٰتِ نَشۡطٗا

Na kwa Malaika ambao huzichukua roho za Waumini kwa uchangamfu na upole. info
التفاسير: |

3 : 79

وَٱلسَّٰبِحَٰتِ سَبۡحٗا

Na kwa Malaika wanaoshuka kutoka mbinguni na kupaa kwenda mbinguni. info
التفاسير: |

4 : 79

فَٱلسَّٰبِقَٰتِ سَبۡقٗا

Na Malaika ambao wanakimbilia kutekeleza amri za Allah Mtukufu. info
التفاسير: |

5 : 79

فَٱلۡمُدَبِّرَٰتِ أَمۡرٗا

Na kwa Malaika wanaopitisha amri za Mola wao katika mambo ya ulimwengu, waliowakilishwa kuyafanya na kuyasimamia, - Wala haifai kwa kiumbe kukiapia chochote kile, bali yapasa kiapo chake kiwe ni kwa jina la Mola wake Muumba au sifa Zake. Na lau ataapa kwa asiye Muumba wake, basi huyo amekuwa mshirikina - Watafufuliwa viumbe bila shaka na watahesabiwa. info
التفاسير: |

6 : 79

يَوۡمَ تَرۡجُفُ ٱلرَّاجِفَةُ

Siku ambayo ardhi itatetemeka kwa Mpulizo wa kwanza. info
التفاسير: |

7 : 79

تَتۡبَعُهَا ٱلرَّادِفَةُ

Mpulizo wa kufisha, ukifuatiwa na Mpulizo mwingine wa kuhuisha. info
التفاسير: |

8 : 79

قُلُوبٞ يَوۡمَئِذٖ وَاجِفَةٌ

Nyoyo za makafiri, Siku hiyo, zitakuwa na papatiko kwa hofu kubwa. info
التفاسير: |

9 : 79

أَبۡصَٰرُهَا خَٰشِعَةٞ

Macho ya makafiri hao yatakuwa madhalilifu kwa kitisho watakachokiona. info
التفاسير: |

10 : 79

يَقُولُونَ أَءِنَّا لَمَرۡدُودُونَ فِي ٱلۡحَافِرَةِ

Wanasema hawa wakanushao kufufuliwa: Je, tutarudishwa baada ya kufa kwetu kwenye yale tuliyokuwa nayo katika ardhi? info
التفاسير: |

11 : 79

أَءِذَا كُنَّا عِظَٰمٗا نَّخِرَةٗ

Je, tutarudishwa na hali tutakua mifupa iliochakaa? info
التفاسير: |

12 : 79

قَالُواْ تِلۡكَ إِذٗا كَرَّةٌ خَاسِرَةٞ

Wakasema: «Kurejea kwetu huko kutakuwa kutupu kusikokuwa kweli». info
التفاسير: |

13 : 79

فَإِنَّمَا هِيَ زَجۡرَةٞ وَٰحِدَةٞ

Hakika tukio hilo litakuwa kwa mpulizo mmoja tu. info
التفاسير: |

14 : 79

فَإِذَا هُم بِٱلسَّاهِرَةِ

Wakitahamaki wako hai juu ya ardhi baada ya kuwa walikuwa ndani yake. info
التفاسير: |

15 : 79

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ

Je imekujilia, (ewe Mtume), habari ya Mûsã? info
التفاسير: |

16 : 79

إِذۡ نَادَىٰهُ رَبُّهُۥ بِٱلۡوَادِ ٱلۡمُقَدَّسِ طُوًى

Pindi Mola wake Alipomwita katika bonde lililotakaswa na kubarikiwa, la Ṭuwā. info
التفاسير: |
prev

An-Nazi'at

next
:
0:00 0:00