prev

Al-Falaq

next

1 : 113

قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلۡفَلَقِ

Sema, (ewe Mtume), «Najilinda na kutaka hifadhi kwa muumbaji wa asubuhi». info
التفاسير: |

2 : 113

مِن شَرِّ مَا خَلَقَ

Kutokana na shari ya viumbe na maudhi yao. info
التفاسير: |

3 : 113

وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ

Na kutokana na shari ya usiku wenye giza kubwa uingiapo na ujikitapo, na kutokana na shari na maudhi mbalimbali yaliyomo ndani yake. info
التفاسير: |

4 : 113

وَمِن شَرِّ ٱلنَّفَّٰثَٰتِ فِي ٱلۡعُقَدِ

Na kutokana na shari za wchawi wenye kupuliza kwenye mafundo wanayoyafunga kwa lengo la kuroga. info
التفاسير: |

5 : 113

وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ

Na kutokana na shari za hasidi mwenye kuchukia watu, anapowahusudu na kuwadhuru, kwa kutaka neema za Allah Mtukufu alizowaneemesha ziwaondokee. info
التفاسير: |
prev

Al-Falaq

next
:
0:00 0:00