prev

Quraish

next

1 : 106

لِإِيلَٰفِ قُرَيۡشٍ

Oneni ajabu ya mazowea ya makureishi, na amani walionayo, na kuwaendea uzuri mambo yao. info
التفاسير: |

2 : 106

إِۦلَٰفِهِمۡ رِحۡلَةَ ٱلشِّتَآءِ وَٱلصَّيۡفِ

Oneni ajabu kwa kupangika na kuwepesika kwa misafara yao ya kwenda yemeni kipindi cha kusi na kwenda Shamu kipindi cha kaskazi, ili kuleta vitu wanavyohitajia, na kuwa yote hayo yamewepesishwa na Allah Mtukufu. info
التفاسير: |

3 : 106

فَلۡيَعۡبُدُواْ رَبَّ هَٰذَا ٱلۡبَيۡتِ

Basi, wamshukuru na kumuabudu Bwana wa Nyumba hii ya Al Ka‘ba, ambayo kwa ajili Yake wamepewa cheo na ukarimu, na wampwekeshe na kumtakasia ibada mola wa nyumba hiyo ya Al Ka‘ba. info
التفاسير: |

4 : 106

ٱلَّذِيٓ أَطۡعَمَهُم مِّن جُوعٖ وَءَامَنَهُم مِّنۡ خَوۡفِۭ

Mola ambaye Amewapa chakula wakati wa njaa kali, na akawapa amani na utulivu dhidi ya hofu iliyokua kubwa sana. info
التفاسير: |
prev

Quraish

next
:
0:00 0:00