prev

Al-Masad

next

1 : 111

تَبَّتۡ يَدَآ أَبِي لَهَبٖ وَتَبَّ

Imepata hasara mikono miwili ya Abū Lahab, na yeye mwenyewe ameangamia, kwa kumuudhi Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). na kwa hakika ilitimia na kutokea hasara ya abû lahab. info
التفاسير: |

2 : 111

مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُۥ وَمَا كَسَبَ

Haikumnufaisha mali yake na watoto wake. Kwani hivyo havitamkinga na adhabu ya Allah Mtukufu. info
التفاسير: |

3 : 111

سَيَصۡلَىٰ نَارٗا ذَاتَ لَهَبٖ

Ataingia kwenye Moto wenye mapande makubwa ya moto yanayochomoza kama ulimi. info
التفاسير: |

4 : 111

وَٱمۡرَأَتُهُۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ

Atauingia moto huo yeye na mke wake ambaye alikuwa akibeba miba na kuiweka kwenye njia anayopita Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), ili kumuudhi. info
التفاسير: |

5 : 111

فِي جِيدِهَا حَبۡلٞ مِّن مَّسَدِۭ

Kwenye shingo yake patakuwa na kamba imara atabebewa nayo kwenye Moto wa Jahanamu, kisha atarushwa nayo mpaka chini. info
التفاسير: |
prev

Al-Masad

next
:
0:00 0:00