قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - عبد اللہ محمد اور ناصر خمیس

صفحہ نمبر:close

6 : 98

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ وَٱلۡمُشۡرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَآۚ أُوْلَٰٓئِكَ هُمۡ شَرُّ ٱلۡبَرِيَّةِ

Hakika wale waliokufuru miongoni mwa Mayahudi na manaswara na Washirikina, mateso yao ni Moto wa Jahanamu. Watakuwa ni wenye kukaa milele humo, Wao ndio viumbe waovu kabisa. info
التفاسير: |

7 : 98

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ أُوْلَٰٓئِكَ هُمۡ خَيۡرُ ٱلۡبَرِيَّةِ

Hakika wale waliomuamini Allah Mtukufu, wakamfuata Mtume wake na wakafanya amali njema, wao ndio viumbe bora. info
التفاسير: |

8 : 98

جَزَآؤُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ جَنَّٰتُ عَدۡنٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۖ رَّضِيَ ٱللَّهُ عَنۡهُمۡ وَرَضُواْ عَنۡهُۚ ذَٰلِكَ لِمَنۡ خَشِيَ رَبَّهُۥ

Malipo yao, mbele ya Mola wao Siku ya Kiyama, ni Pepo ya makazi na utulivu, yenye upeo wa uzuri, ambayo chini ya majumba yake ya fahari inapita mito; watakaa milele humo. Allah Mtukufu Ameridhika nao, Akakubali amali zao njema. Na wao wameridhika naye kwa mapokezi Aliyowafanyia ya aina mbalimbali za takrima. Malipo mazuri hayo ni ya aliyemuogopa Mweyezi Mungu na akajiepusha na maasi. info
التفاسير: |
next

Al-Bayyinah

prev
:
0:00 0:00