Prijevod značenja Plemenitog Kur'ana - Prevod na svahili jezik - Abdullah Muhammed i Nasir Hamis

Broj stranice:close

91 : 15

ٱلَّذِينَ جَعَلُواْ ٱلۡقُرۡءَانَ عِضِينَ

«Na wao ni wale walioifanya Qur’ani kuwa ni vigawanyo na mafungu.» Kati yao kuna wanaosema, ‘ni uchawi’ na kati yao kuna wanaosema, ‘ni ukuhani’ na kati yao kuna wanaosema yasiyokuwa hayo ili wawazuie watu kufuata uongofu. info
التفاسير: |

92 : 15

فَوَرَبِّكَ لَنَسۡـَٔلَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Naapa kwa Mola wako, tutawahesabu tena tutawahesabu Siku ya Kiyama, na tutawalipa tena tutawalipa wote kwa kuigawanya kwao Qur’ani, kwa kuzua kwao urongo, kuibadilisha, kuipotoa na yasiyokuwa hayo. info
التفاسير: |

93 : 15

عَمَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Ambayo wao walikuwa wakiyatenda ya kuabudu mizimu, maasia na madhambi. Na katika haya pana kuwaonya wao wasidumu nayo haya matendo mabaya. info
التفاسير: |

94 : 15

فَٱصۡدَعۡ بِمَا تُؤۡمَرُ وَأَعۡرِضۡ عَنِ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Na utangaze waziwazi ulinganizi wa haki ambao Amekuamrisha nao Allah Mtukufu, wala usiwajali washirikina, kwani kwa kweli Amekutakasa Allah Mtukufu kutokana na hayo wanayoyasema. info
التفاسير: |

95 : 15

إِنَّا كَفَيۡنَٰكَ ٱلۡمُسۡتَهۡزِءِينَ

Sisi, kwa hakika, tumekutosheleza hao wacheza shere wenye kufanya dharau kati ya viongozi wa Kikureshi. info
التفاسير: |

96 : 15

ٱلَّذِينَ يَجۡعَلُونَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۚ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ

Ambao wameifanya mizimu na vinginevyo kuwa ni washirika wa Allah Mtukufu. Basi watakuja kuujua mwisho wa vitendo vyao, hapa duniani na kesho Akhera. info
التفاسير: |

97 : 15

وَلَقَدۡ نَعۡلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدۡرُكَ بِمَا يَقُولُونَ

Na kwa kweli, tunaujua unyongekaji wa kifua chako, ewe Mtume, kwa yale wayasemayo washirikina kuhusu wewe na kuhusu ulinganizi wako. info
التفاسير: |

98 : 15

فَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ وَكُن مِّنَ ٱلسَّٰجِدِينَ

Kimbilia kwa Mola wako pindi unaponyongeka moyo wako, na mtakasie yeye kwa kumshukuru na kumsifu. Na uwe ni miongoni mwa wenye kuswali kwa ajili ya Allah Mtukufu na wenye kumuabudu, kwani kwa kweli hilo litakutosheleza na lile lenye kukutia kero. info
التفاسير: |

99 : 15

وَٱعۡبُدۡ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأۡتِيَكَ ٱلۡيَقِينُ

Na uendelee kumuabudu Mola wako muda wa uhai wako mpaka ikujie yakini isiyokuwa na shaka nayo ni kifo. Na Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), alitekeleza amri ya Mola Wake, kwani hakuacha kuendelea kumuabudu Allah Mtukufu mpaka ikamjia yakini ya kifo kutoka kwa Mola Wake. info
التفاسير: |
prev

Al-hijr

next
:
0:00 0:00