prev

Az-Zalzalah

next

1 : 99

إِذَا زُلۡزِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ زِلۡزَالَهَا

Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu. info
التفاسير: |

2 : 99

وَأَخۡرَجَتِ ٱلۡأَرۡضُ أَثۡقَالَهَا

Na ikatoa vilivyomo ndani yake: miongoni mwa wafu na thamani za ardhini kama dhahabu na mfano wake. info
التفاسير: |

3 : 99

وَقَالَ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا لَهَا

Na akauliza binadamu, katika hali ya kubabaika, «imepatwa na nini?» info
التفاسير: |

4 : 99

يَوۡمَئِذٖ تُحَدِّثُ أَخۡبَارَهَا

Siku hiyo (siku ya kiama) ardhi itatoa habari ya mambo iliyofanyiwa ya uzuri na ubaya. info
التفاسير: |

5 : 99

بِأَنَّ رَبَّكَ أَوۡحَىٰ لَهَا

Kwa kuwa Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, ataiamuru itoe habari ya mambo iliyofanyiwa. info
التفاسير: |

6 : 99

يَوۡمَئِذٖ يَصۡدُرُ ٱلنَّاسُ أَشۡتَاتٗا لِّيُرَوۡاْ أَعۡمَٰلَهُمۡ

Siku hiyo watu wataondoka kutoka kwenye kisimamo cha Hesabu kwa makundi, ili Allah Mtukufu Awaoneshe waliyoyatenda, mazuri na mabaya, na Awalipe kwayo. info
التفاسير: |

7 : 99

فَمَن يَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةٍ خَيۡرٗا يَرَهُۥ

Yoyote mwenye kufanya jema hata kama ni kwa uzito wa Mdudu Chungu atayaona malipo yake Akhera. info
التفاسير: |

8 : 99

وَمَن يَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةٖ شَرّٗا يَرَهُۥ

Na yoyote mwenye kufanya baya hata kama ni kwa uzito wa Mdudu Chungu atayaona malipo yake Akhera. info
التفاسير: |
prev

Az-Zalzalah

next
:
0:00 0:00