next

Al-Ma'un

prev

1 : 107

أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يُكَذِّبُ بِٱلدِّينِ

Je, umeiona hali ya yule ambaye anakanusha kufufuliwa na kulipwa? info
التفاسير: |

2 : 107

فَذَٰلِكَ ٱلَّذِي يَدُعُّ ٱلۡيَتِيمَ

Huyo ndiye yule anayemkaripia yatima kwa nguvu, akimnyima haki zake kwa sababu ya ususuavu wa moyo wake. info
التفاسير: |

3 : 107

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ

Na wala hawahimizi wengine kulisha masikini. Vipi yeye mwenyewe atamlisha? info
التفاسير: |

4 : 107

فَوَيۡلٞ لِّلۡمُصَلِّينَ

Basi adhabu kali itawafikia wenye kuswali. info
التفاسير: |

5 : 107

ٱلَّذِينَ هُمۡ عَن صَلَاتِهِمۡ سَاهُونَ

Nao ni wale ambao wameghafilika na Swala zao: hawazisimamishi kama ipasavyo wala hawaziswali kwa nyakati zake. info
التفاسير: |

6 : 107

ٱلَّذِينَ هُمۡ يُرَآءُونَ

Na ambao huonyesha watu amali zao za kheri kwa njia ya ria. info
التفاسير: |

7 : 107

وَيَمۡنَعُونَ ٱلۡمَاعُونَ

Na wanakataa kuwaazima watu vitu ambavyo hawadhuriki kwa kuviazima, kama vyombo vya kutumia, na vinginevyo. Wao hawakujifanyia wema nafsi zao kwa kumuabudu Mola wao, wala hawakuwafanyia wema viumbe Vyake. info
التفاسير: |
next

Al-Ma'un

prev
:
0:00 0:00