prev

Al-Ma'un

next

1 : 107

أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يُكَذِّبُ بِٱلدِّينِ

Je, waiona hali ya yule ambaye akanusha kufufuliwa na kulipwa? info
التفاسير: |

2 : 107

فَذَٰلِكَ ٱلَّذِي يَدُعُّ ٱلۡيَتِيمَ

Huyo ndiye yule anayemkaripia yatima kwa nguvu akimnyima haki yake kwa sababu ya ususuavu wa moyo wake. info
التفاسير: |

3 : 107

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ

Na wala hawahimizi wengine kulisha masikini. Vipi yeye mwenyewe atamlisha?. info
التفاسير: |

4 : 107

فَوَيۡلٞ لِّلۡمُصَلِّينَ

Basi adhabu kali itawafikia wenye kusali, info
التفاسير: |

5 : 107

ٱلَّذِينَ هُمۡ عَن صَلَاتِهِمۡ سَاهُونَ

ambao wameghafilika na Swala zao: hawazisimamishi kama ipasavyo wala hawazisali kwa nyakati zake. info
التفاسير: |

6 : 107

ٱلَّذِينَ هُمۡ يُرَآءُونَ

Ambao huonyesha watu amali zao za kheri kwa njia ya ria. info
التفاسير: |

7 : 107

وَيَمۡنَعُونَ ٱلۡمَاعُونَ

Na wanakataa kuwaazima watu vitu ambavyo hawadhuriki kwa kuviazima, kama vyombo vya kutumia na vinginevyo. Wao hawakujifanyia wema nafsi zao kumuabudu Mola wao wala hawakuwafanyia wema viumbe Vyake. info
التفاسير: |
prev

Al-Ma'un

next
:
0:00 0:00